Chama cha mawakili LSK kinatoa wito kwa serikali kupitia upya agizo lake la kuwazuia raia wa kigeni kujihusisha na aina fulani za biashara ndogo. LSK inasema Kenya ina haki ya kudhibiti biashara na kutekeleza sheria za uhamiaji, lakini lazima iheshimu Katiba na majukumu yake chini ya Mkataba wa EAC na Itifaki ya Soko la Pamoja. LSK inasema vikwazo vinapaswa kulenga ukiukwaji maalum na sio kutegemea utaifa pekee. Wakati huo huo, Mbunge wa Kabuchai Majimbo anataka serikali ihakikishe kwamba haki za wageni walioathiriwa zinalindwa.

MAJIMBO KALASINGA – GOV’T