Siku ya Kuzuia Kujitoa uhai Duniani inaadhimishwa hii leo chini ya kaulimbiu, "Kubadilisha simulizi kuhusu kujiua." Kampeni hiyo inahimiza serikali na taasisi kuweka kipaumbele kuzuia kujiua na afya ya akili kupitia mikakati inayotegemea ushahidi na upatikanaji zaidi wa huduma bora. Shirika la afya duniani WHO linasema mawazo ya kujiua mara nyingi huashiria maumivu makali ya kihisia, si udhaifu. Yanahimiza kusikiliza bila hukumu, kuonyesha huruma na kuwasaidia watu walio katika dhiki kutafuta msaada.