Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, ameiomba kamati ya usalama ya Seneti kuchunguza hali ya maisha ya wakimbizi katika kambi zote za wakimbizi nchini, ikiwemo Kakuma. Akizungumza bungeni, Sifuna alionya kuwa mazingira duni yasiyofaa kwa binadamu na kupuuzwa kwao kunaweza kuwasukuma wakimbizi walio katika mazingira magumu kujiunga na makundi ya uhalifu.
EDWIN SIFUNA - REFUGEES