Maafisa wa serikali nchini na washirika wa kimataifa wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi leo ili kujadili sera na mchakato wa mpito kuelekea nishati safi barani Afrika. Mkutano huo unafanyika wakati ambapo zaidi ya Waafrika milioni 600 bado hawana uhakika wa kupata umeme. Miongoni mwa wazungumzaji watakao kuwepo ni Mjumbe Maalumu wa Kenya kuhusu Masuala ya hali ya hewai, Ali Mohammed, na Waziri wa Mazingira, Deborah Barasa. Majadiliano yatalenga kufungua fursa za nishati endelevu barani Afrika ili kusaidia uundaji wa ajira, ukuaji wa viwanda na ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.