Wakenya waliokuwa wakielekea kazini asubuhi ya leo kupitia Barabara ya Thika walikwama katika msongamano mkubwa wa magari kwa zaidi ya saa moja kati ya Ruiru Bypass na Githurai 45, kufuatia ajali ndogo iliyohusisha gari aina ya 'pickup' lililokuwa likisafirisha mayai eneo la Githurai 45. Ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa, huku madereva wakilazimika kusubiri kwa saa kadhaa wakati magari yaliyokuwa yakipita kwa kwando yakizidisha msongamano na kuleta vurugu kwenye barabara hiyo kuu yenye shughuli nyingi.