Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane, ni mmoja wa wachezaji watatu wa Uingereza walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya mwaka 2026. Jude Bellingham wa Real Madrid na Declan Rice wa Arsenal wanajiunga na Kane, kwenye orodha ya wachezaji 30 walioteuliwa. Washambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe na Vinicius Junior pia wameorodheshwa, pamoja na mabeki wa Arsenal, Gabriel na William Saliba. Washindi wa ligi ya mabingwa PSG walitoa idadi kubwa zaidi ya walioteuliwa huku Ousmane Dembélé, Achraf Hakimi, Khvicha Kvaratskhelia, Marquinhos, Nuno Mendes, João Neves Vitinha na Willian Pacho wote kutoka PSG wakiorodheshwa.
Lamine Yamal anajiunga na mwenzake wa timu ya Bracelona, Pau Cubarsí, huku Michael Olise wa Bayern Munich na Dayot Upamecano pia wakiteuliwa.
Lionel Messi wa Inter Miami alijitosa kwenye orodha hiyo kwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye Kombe la Dunia akiwa na Argentina, lakini hakuna nafasi kwenye orodha ya walioteuliwa kwa mpinzani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo. Hata hivyo, kuna nafasi ya mshambuliaji mwingine wa Al Nassr, Sadio Mané na Julián Quiñones wa Al Qadsiah.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisii, Kitale na Kericho.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.