Serikali imehimizwa kutathmini hali ya misitu ya Kenya kabla ya mvua kubwa inayotarajiwa ya El Niño ili kulinda miti iliyopandwa kama sehemu ya juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya anga. Mkurugenzi Mkuu wa Vijana wa Kilifi, Emmanuel Gonna, anasema serikali bado haijatoa taarifa kuhusu maandalizi katika misitu ili kuhakikisha miti iliyopandwa hivi karibuni haiharibiwi na mvua kubwa. Gonna anasema kulinda miche hiyo itakuwa muhimu katika kuendeleza juhudi za Kenya za kupanda miti upya na kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa.


EMMANUEL GONNA – ELNINO