Seneta Mteule Catherine Mumma ametoa wito wa kuanzishwa kwa idara maalum ndani ya Wizara ya Mambo ya kigeni ili kushughulikia Unyanyasaji wa Kijinsia (GBV). Akizungumza katika Jukwaa la Kitaifa la Kumaliza Tishio la Mara Tatu jijini Nairobi, Mumma alisema Kenya inapaswa kusonga mbele zaidi ya ulinzi tendaji na kuanzisha vitengo maalum vilivyoratibiwa ndani ya vyombo vya usalama na utekelezaji wa sheria. Pendekezo lake linaendana na agizo la Waziri Kipchumba Murkomen kwa vituo vyote vya polisi kudumisha madawati ya jinsia yanayofanya kazi ili kushughulikia kesi za GBV kitaaluma.


CATHERINE MUMMA – DEPARTMENT