Spika wa Seneti Amason Kingi anasema maandalizi yako katika hatua ya juu kwa Maseneta kufanya vikao vya jumla na kamati katika Kaunti ya Kilifi kuanzia Septemba tarehe 21 hadi 25. Kingi anasema mpango huo utajumuisha mikutano ya kamati na ziara za usimamizi wa miradi mbalimbali ya serikali ya kitaifa katika kaunti hiyo. Anasema maelezo zaidi kuhusu mpango huo yatawasilishwa kupitia Ofisi ya Karani huku maandalizi yakiendelea kwa vikao hivyo.
AMASON KINGI – SITTINGS