Rais William Ruto amemwagiza Mdhibiti wa Bajeti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuunga mkono serikali za kaunti katika kuthibitisha, kuorodhesha na kuharakisha kilpwa kwa madeni yanayosubiriwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Ruto alisema madeni ambayo hayajalipwa yanavunja biashara, kuharibu maisha na kufifisha imani ya umma. Alionya kwamba madeni haya yanaweza kusababisha usumbufu wa biashara na kuziacha kaunti zikiwa na matatizo ya kifedha huku nchi ikiingia katika kipindi cha uchaguzi.


WILLIAM RUTO - BILLS