Rais William Ruto anaanza ziara ya siku nne ya maendeleo huko South Rift hii leo, akitembelea kaunti za Bomet na Kericho. Huko Bomet, miongoni mwa mambo mengine atatembelea Uwanja wa Ndege wa Itembe, kuzindua Hospitali ya Mama na Mtoto ya Joyce Laboso na kuzindua Mradi wa Nyumba za Bei Nafuu wa Chepalungu. Ijumaa, Ruto atawashirikisha wakaazi na kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo bunge ya Kapsoit, Kapkatet na Kipkelion Mashariki katika Kaunti ya Kericho.