Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed anasema ODM itabaki katika serikali pana hadi mwisho wa muhula wa Rais William Ruto. Junet alimshutumu Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua na wakosoaji wengine kwa kujaribu kuiondoa ODM serikalini. Alisema ODM itafanya kazi na washirika wake wa muungano ili kuunda serikali ijayo, akipuuza kile alichokiita majaribio ya kudhoofisha ushirikiano huo.


JUNET MOHAMED – SERIKALI