Seneta wa Kakamega Boni Khalwale anataka Kamati ya Elimu ya Seneti imwite Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula kutokana na madai kwamba wabunge huchukua barua za kuajiri walimu kutoka Ikulu. Khalwale anasema madai hayo ni mazito na Wetang'ula anapaswa kufika mbele ya kamati hiyo ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo. Seneta huyo anasema kamati hiyo inapaswa kubaini jinsi barua zinazodaiwa za kuajiri zinavyotolewa na jukumu la wabunge katika mchakato huo.
BONI KHALWALE – WETANGULA