Mwenyekiti wa Kitaifa wa ODM Gladys Wanga ameshutumu upinzani kwa kukosa ajenda kwa Wakenya. Akizungumza katika Chungwa House, Gavana huyo wa Homa Bay aliwasihi Wakenya kutowatilia maanani viongozi anaosema wanapanga siasa za mgawanyiko. Wanga alisema ODM na serikali pana itaendelea kutetea ujumuishaji, huku akihimiza jamii ya Maa kubaki imara katika chama hicho.

GLADYS WANGA – OPPOSITION