Wauguzi na wakunga waliogoma wanatarajiwa kurudi mitaani leo huku wakishinikiza kutatuliwa kwa malalamiko yao. Katika taarifa kwa polisi, Chama cha Wauguzi na Wakunga cha Kenya kinasema wanachama wake watakusanyika Greenpark jijini Nairobi kabla ya kuandamana kando ya Waiyaki Way hadi makao makuu ya Baraza la Magavana huko Westlands. Ripoti ya hivi karibuni ya KNCHR ilisema vifo vya angalau 79 vimehusishwa na mgomo huo. Chama cha madaktari KMPDU kimetoa notisi ya siku 7 ya mgomo kwa serikali ili kutatua mgomo huo.

DAVJI ATELLAH – STRIKE