Kuna wito wa sheria au miongozo iliyo wazi kuhusu kutoa dawa za kuzuia mimba kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18. Mwanagainakolojia Davis Kibii anasema ukosefu wa uwazi unaleta changamoto kwa madaktari, licha ya kuongezeka kwa visa vya mimba za utotoni na utoaji mimba usio salama ambavyo vinaweza kupunguzwa kupitia upatikanaji wa dawa za kuzuia mimba. Anasema kuna haja ya majadiliano ya wazi kuhusu matumizi ya njia za kuzuia mimba miongoni mwa watoto ili kushughulikia tatizo hilo kwa ufanisi.
DAVIS KIBII – MINORS