Timu za netiboli za wanaume na wanawake za Kenya zimeimarisha mazoezi katika uwanja wa Kasarani kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Netiboli la Afrika litakaloanza tarehe 19-26 mwezi huu. Timu ya wanaume ya Kenya inafundishwa na Peter Oloo huku Evelyn Cherono akiongoza timu ya wanawake huku kocha wa Zimbabwe Tapiwa Chirenda akisaidia timu zote mbili. Wenyeji Kenya watakabiliana na Afrika Kusini, Malawi, Namibia, na Nigeria katika Kundi A, huku Kundi B likiwa na Uganda, Zimbabwe, Zambia, Botswana na Tanzania. Droo ya wanaume itafanyika leo.
Anga kavu na kijibaridi zinashuhudiwa Naivasha, Gilgil na Nakuru.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.