Rais William Ruto ameidhinisha Muswada wa Marekebisho wa Usimamizi wa Fedha za Umma wa 2025, unaolenga kuimarisha uwajibikaji wa kifedha na ushiriki wa umma. Sheria hiyo inatoa uwasilishaji wa makato ya kisheria kwa wakati unaofaa, inayataka mabunge ya kaunti kupitisha Miswada ya Fedha kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha, na inapunguza kipindi cha taasisi za umma kuwasilisha taarifa za fedha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kutoka miezi mitatu hadi miwili. Pia inaongeza muda wa kuzingatia Taarifa ya Sera ya Bajeti kutoka siku 14 hadi 21. Rais pia alitia saini mswada wa baraza la kitaifa la idadi ya watu na maendeleo, mswada wa marekebisho wa huduma ya abiria wa anga na muswada wa usimamizi wa amana.

 

SAMUEL NJOROGE -BILL