Raia wote wasio na vibali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa raia wa Burundi wanaoishi Kenya, wameagizwa kujitokeza katika balozi zao kwa ajili ya usajili rasmi wa vitambulisho. Msemaji wa Serikali Charles Owino anasema Wizara ya Mambo ya kigeni itawasiliana na Ubalozi wa Burundi na washirika wengine wa kikanda ili kurasimisha na kusimamia kesi hizo. Hii inafuatia agizo la hivi karibuni la Rais William Ruto kuhusu raia wa kigeni wanaojihusisha na biashara ndogo.
CHARLES OWINO – REGISTRATION