Muungano wa Jumuiya za Kiafrika Zinazoshughulikia Mabadiliko ya Hali ya hewa unatoa wito kwa afya ya akili kujumuishwa katika mipango ya kujiandaa na hali ya hewa na majanga. Akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya hali ya hewa huko Isinya, Kaunti ya Kajiado, Mshauri Mtendaji Rosalid Nkirote alisema mafuriko na mishtuko mingine ya hali ya hewa sio tu kwamba huharibu mali bali pia huathiri ustawi wa kiakili na kihisia wa watu. Warsha hiyo inajadili maandalizi ya mvua fupi za Oktoba-Desemba.