Katibu Afya ya Umma Mary Muthoni amesema Kenya haina visa vilivyothibitishwa vya Ebola. Muthoni amesema Wizara ya Afya imeweka hatua za kugundua na kudhibiti visa vyovyote vinavyoshukiwa. Aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali inaendelea kuzingatia kuzuia virusi hivyo kuingia nchini na kuimarisha utayari wa kukabiliana na maambukizi yoyote yanayoshukiwa.
MARY MUTHONI-EBOLA