Kamati ya Hesabu za Umma ya Seneti imemwalika tena Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuelezea ni kwa nini polisi wameshindwa kumkamata Gavana wa Isiolo Abdi Guyo na kumwasilisha mbele ya kamati hiyo. Kanja alikosa mkutano wa jana, akitaja safari rasmi nchini Uchina, sababu ambayo maseneta waliikataa. Kamati hiyo inasema gavana amepuuza wito mara kwa mara. Maseneta pia waliamua kuandaa ripoti maalum kuhusu fedha za Isiolo, ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa kisayansi uliopendekezwa.