Gavana wa Mombasa Abdullswamad Nassir anasema kaunti inaweka hatua za kujiandaa kwa hali inayotarajiwa ya El Niño. Gavana huyo aliwasihi wakaazi kuendelea kuwa macho na kuchukua tahadhari zinazohitajika, hasa wale wanaoishi karibu na vyanzo vya maji na maeneo yanayokumbwa na mafuriko. Amewashauri wakaazi katika maeneo kama hayo kuhamia maeneo ya juu ili kuepuka uwezekano wa kupoteza maisha na mali.

ABDULLSWAMAD NASSIR – EL NINO