Chama cha Wanatiba wa Viungo cha Kenya leo kitafanya matembezi kutoka hospitali ya KNH kuadhimisha Siku ya Tiba ya Viungo Duniani. Rais wa Chama hicho Erastus Osewe anasema tukio hilo litaongeza uelewa kuhusu jukumu la tiba ya viungo na shughuli za kimwili katika kuzuia, kudhibiti na kurekebisha magonjwa ya moyo na mishipa na kiharusi. Mada ya Siku ya Tiba ya Viungo Duniani ya mwaka huu inalenga jukumu la tiba ya viungo katika kushughulikia magonjwa ya moyo na mishipa na kiharusi.
ERASTUS OSEWE - WALK