Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewaonya wahuni dhidi ya kutumiwa kuvuruga mkutano mkuu wa vuguvugu la Linda Mwananchi jijini Nairobi wikendi hii. Aliwasihi wale wanaopanga kuhudhuria mkutano huo kufanya hivyo kwa amani na kuonya dhidi ya kutumiwa kusababisha machafuko. Mbunge huyo pia alitishia kuwafichua wabunge kadhaa wa Nairobi ambao aliwashutumu kwa kutumiwa kuchochea vurugu na kuwatumia wahuni kuvuruga shughuli za kisiasa.
BABU OWINO – GOONS