Wakenya wamehimizwa kuwa macho sana huku Wizara ya Afya ikiibua wasiwasi kuhusu tishio linaloendelea kutokana na virusi vya Mpox. Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni anasema virusi hivyo bado vipo kimya kimya katika jamii, hasa karibu na mipaka, na kuwasihi Wakenya kuchukua tahadhari zinazohitajika. Muthoni, ambaye alitoa taarifa mpya kuhusu hali, alibaini kuwa wagonjwa wa Mpox wanaendelea kutibiwa katika wodi za kutengwa kote nchini.

MARY MUTHONI –MPOX