Shirika la afya duniani linaonya kuhusu hatari kubwa za kiafya na kimazingira zinazohusiana na kilimo cha tumbaku barani Afrika. WHO inasema wakulima wanakabiliwa na magonjwa yanayosababishwa na kuathiriwa na nikotini, dawa za kuuwa wadudu na vumbi la tumbaku, huku kilimo kikichangia uharibifu wa udongo, ukataji miti na matumizi makubwa ya maji. Pia inahusishwa na ajira kwa watoto katika baadhi ya jamii maskini. Shirika hilo linatoa wito wa usaidizi zaidi ili kuwasaidia wakulima kuhamia kwenye njia mbadala endelevu za kujipatia riziki.