Zaidi ya wataalamu elfu 11 wa teknolojia ya famasia wametishia kugoma wakipinga miongozo mipya ambayo ingewazuia kufanya kazi katika vituo vya afya vya Level 3 hadi 6. Mwenyekiti wa Chama cha Famasia cha Kenya Chitechi Amboka aliita miongozo hiyo, kuwa ya kibaguzi, akisema sheria hizo zinawanyima wenye diploma waliohitimu haki ya kushughulikia dawa muhimu. Chini ya miongozo hiyo mipya iliyopitishwa na Bodi ya Famasia, ni wataalamu wenye sifa za kiwango cha shahada pekee, ndio watakaoruhusiwa kutoa dawa katika vituo vilivyotajwa, huku wenye diploma wakisimamia zahanati.