Huenda upinzani ukamtangaza mgombea wake wa urais mwezi Machi mwaka ujao. Hii ni kulingana na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua ambaye alisema upinzani hauko chini ya shinikizo la kufichua mpeperusha bendera wake, akipuuza wito wa viongozi wanaounga mkono serikali wa kutaka tangazo la mapema. Gachagua alisema mashauriano na majadiliano miongoni mwa wakuu wa upinzani yanaendelea, huku viongozi wote wakiwa wamejitolea kumuunga mkono yeyote atakayechaguliwa.
RIGATH GACHAGUA-CANDIDATE