Mabingwa wa rekodi wa KPL, Gor Mahia, lazima waifunge Pyramids FC kwa angalau mabao mawili bila jibu katika mechi ya pili wa awali wa ligi ya mabingwa wikendi ijayo jijini Cairo, ili kudumisha nafasi yao ya raundi ya pili baada ya kufungwa 2-0 na Wamisri katika uwanja wa Nyayo jana. Walid El Karti aliiweka Pyramids mbele katika dakika ya tano, kabla ya Mahmoud Saber kuongeza la pili kabla ya mapumziko. KO'gallo walipambana vikali kuokoa sare lakini Pyramids walijilinda vyema na kushikilia uongozi.
Wakati huo huo, washindi wa kombe la FKF, Tusker FC, walitoka sare ya 2-2 na Al Ahli Madani katika mechi yao ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho la CAF katika Uwanja wa Pele Kigali. Victor Mbaoma na Abdoulie Joof waliweka Tusker uongozini katika dakika ya 11 na 46, lakini mabao mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Samani Al-Sawi yaliharibu mchezo. Tusker wanahitaji angalau sare tasa katika mechi ya marudio katika uwanja wa Nyayo wikendi ijayo, ili kufuzu kwa raundi ya pili kwa mabao ya ugenini.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kericho, Kitale na Kisii.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.