Ni faraja kwa wakaazi wa Kajiado kufuatia kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya Barabara ya Kahara-Ngong. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo, Rais William Ruto alisema barabara hiyo ya kilomita 2.8 itapanuliwa hadi Barabara ya Magadi ili kurahisisha usafiri na kuboresha muunganisho. Aliongeza kuwa serikali imejitolea kujenga barabara zaidi katika Kaunti ya Kajiado, pamoja na nyumba za bei nafuu na miradi mingine ya maendeleo.
WILLIAM RUTO-ROAD