Polisi jijini Nairobi wameonya umma dhidi ya kuwalenga wageni wanaodhaniwa kuwa nchini bila idhini, wanaojihusisha na biashara ndogo. Polisi wanasema hawajapokea ripoti zozote za unyanyasaji dhidi ya wageni hao hasa kutoka Congo, Burundi na Rwanda. Polisi waliongeza kuwa pia hawajapokea ripoti zozote za kuhama kwa wageni hao. Hii inafuatia ripoti za mitandao ya kijamii kwamba wageni wengi walikuwa wakiondoka nchini kwa barabara.