Msako mkali dhidi ya raia wa kigeni wanaojihusisha na shughuli za uchuuzi na biashara ndogo nchini unatarajiwa kufanyika leo huku serikali ikichukua hatua za kuwalinda wafanyabiashara wa ndani kutokana na ushindani usio wa haki. Msako huo uliamriwa na Rais William Ruto ambaye alitaj wasiwasi uliotolewa na wafanyabiashara wa ndani kwamba baadhi ya wageni wameanzisha biashara, wakishindana moja kwa moja na wachuuzi wa ndani na wafanyabiashara wadogo. Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba Serikali kufikiria upya agizo la kuwaondoa.

VOX POP – RECONSIDER