Idara ya utabiri wa hali ya hewa amesema wakulima wana takriban wiki tatu za kukamilisha kuvuna, kukausha mazao yao na kuandaa mashamba yao kabla ya mvua ya El Nino kuanza katika maeneo mengi. Idara hiyo inasema Septemba kwa ujumla itaendelea kuwa na jua na ukavu katika sehemu nyingi nchini. Hali ya ukavu huwapa wakulima dirisha muhimu la kumaliza kuvuna na kukausha mazao yao ipasavyo kabla ya msimu wa mvua wa Oktoba-Novemba-Desemba kuanza. Onyo hilo ni muhimu hasa kwa wakulima ambao bado wana mahindi na mazao mengine mashambani.