Mamia ya raia wa Burundi wamemiminika kwenye ubalozi wao jijini Nairobi kupata hati za usafiri wa dharura wanapojiandaa kurudi nyumbani. Ubalozi wa Burundi umeanza kutoa hati za usafiri wa dharura bila malipo kwa raia wanaotaka kuondoka Kenya. Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya serikali ya Kenya kutangaza msako mkali dhidi ya wahamiaji wasio na vibali wanaofanya kazi nchini humu. Burundi pia imeonya Kenya kwamba kuendelea kutoa hotuba za chuki zinazowalenga raia wake kunaweza kuharibu uhusiano kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki.