Rais William Ruto ametangaza kwamba serikali haitasafirisha tena malighafi na madini yote yatasafishwa humu nchini. Alisema kwamba serikali itachunguza chaguo la kusindika madini yote ikiwa ni pamoja na dhahabu, chokaa au limestone, madini ya chuma, graphite, titanium, soda ash, akibaini kuwa itatoa fursa za ajira kwa wengi na kuongeza thamani ya mtaji kwa taifa.