Kaimu Katibu Mkuu wa ODM Catherine Omanyo amewasilisha upya changamoto yake kwa Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku ya kujiondoa katika chama hicho ikiwa hajaridhika. Omanyo alipuuza madai ya awali ya Lenku kwamba chama hicho hakijafanya chochote kwa jamii ya Wamaasai, akiwaambia wakaazi kwamba jamii hiyo imefaidika pakubwa na Serikali pana ya Rais William Ruto, ambayo alisema imewazawadia Wamaasai kwa uteuzi wa juu katika serikali.

 

CATHERINE OMANYO – LENKU