Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua amesisitiza kwamba viongozi wa upinzani wataungana nyuma ya mgombea mmoja wa urais ili kumpinga Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027. Akizungumza na Wakenya nchini Marekani, Gachagua alitetea ziara yake inayoendelea Marekani, akisema itamruhusu kufanya maamuzi na mikakati mizuri ya kisiasa katika kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao.
RIGATHI GACHAGUA-UNITE