Katibu Mkuu wa baraza la makanisa nchini NCCK Chris Kinyanjui anawashutumu polisi kwa kutekeleza sheria dhidi ya wanasiasa kiubaguzi, kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao. Kinyanjui anataja kukamatwa kwa mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia na kikosi kikubwa cha maafisa, huku akihoji ukosefu wa hatua kama hiyo dhidi ya mbunge wa Homa Bay mjini Peter Kaluma kuhusu matamshi anayosema yalihusishwa na vurugu. Kinyanjui anataka polisi, NCIC na waendesha mashtaka kutenda bila upendeleo dhidi ya wanasiasa wote.

CHRIS KINYANJUI – INSTITUTIONS