Askofu Margaret Wanjiru ametangaza rasmi nia yake ya kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 kwa tiketi ya chama cha Kenya Moja Movement (K1). Wanjiru alisema uamuzi wake ulifuatia mashauriano na wafuasi wake, washirika wa kisiasa na wadau wengine, ambao alisema wamemsihi kutoa mwelekeo kuhusu hatua yake ijayo ya kisiasa.
MARGARET WANJIRU - GOVERNOR