Wapelelezi wanachunguza tukio ambapo afisa mkuu wa Huduma ya Magereza nchini alipatikana amefariki ndani ya gari lake huko Juja, kaunti ya Kiambu. Msimamizi Mkuu wa Magereza (SSP) Eric Wainaina mwenye umri wa miaka 40, anayehudumu katika Makao Makuu ya Huduma ya Magereza huko Nyeri, alipatikana jana asubuhi. Polisi walisema umma uliripoti kuugundua mwili huo kwa kupiga simu yapata saa nne unusu asubuhi.