Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Utawala Gilbert Masengeli amewasihi maafisa wapya wa Polisi wa Utawala kuzingatia weledi, utawala wa sheria, haki za binadamu na nidhamu wanapoanza kuitumikia nchi. Akizungumza wakati wa gwaride la kuhitimu mafunzo ya APS huko Embakasi Masengeli pia aliwataka umma kuwakaribisha maafisa hao wapya na kushirikiana nao katika kuimarisha usalama. Alisisitiza kwamba kudumisha usalama ni jukumu la pamoja kati ya polisi na umma.

GILBERT MASENGELI-PROFESSIONAL