Mke wa Rais mama Rachel Ruto ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika ustawi na elimu ya watoto wenye mahitaji maalum, akisema kila mtoto anastahili fursa nzuri ya kujifunza, kukua na kufanikiwa. Akizungumza wakati wa ziara yake katika Shule ya walemavu wa kusikia ya St Luke huko Mbeere Kusini, Kaunti ya Embu, Mama Rachel alisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika watoto wenye mahitaji maalum ya kielimu, akiuita uwekezaji katika mustakabali wa Kenya.
RACHEL RUTO - INVEST