Wanawake wanaweza kudumisha, kuongoza na kubadilisha jamii wanapowezeshwa kiuchumi na kuungwa mkono, Mke wa rais Mama Rachel Ruto amesema. Akiongea wakati wa Mikutano ya kuwezesha Wanawake katika kaunti za Embu na Kirinyaga, Mama Rachel alisema kuwekeza katika uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake ni mojawapo ya njia za uhakika za kuimarisha familia na jamii. Alisema hii huwapa wanawake heshima na uhuru wa kuhudumia familia zao, kukuza biashara na kutumia fursa zinazoibuka.

RACHEL RUTO - EMPOWERMENT