Rais William Ruto ameiagiza KRA kuregesha kiwango cha Sh milioni 2.5 kwa shehena ya jumla iliyounganishwa kwenye makontena, na kubatilisha ongezeko la hivi karibuni la hadi Sh milioni 3.2 . Ruto alitoa agizo hilo jana alipokuwa akiwakaribisha wafanyabiashara wa biashara ndogo ndogo katika Ikulu, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za juu zinazohusiana na uagizaji. Pia ameiagiza KRA kukusanya orodha ya bidhaa zenye thamani kubwa ambazo hazistahili kuunganishwa na kwa hivyo hazitatozwa kikomo cha Sh2.5 milioni.
WILLIAM RUTO - VALUE