Rais William Ruto anatarajiwa kuzuru Kaunti ya Kajiado hii leo hadi Jumamosi huku maendeleo yakiwa ajenda muhimu ya ziara hiyo. Rais atakagua miongoni mwa mambo mengine Barabara ya Rombo-Taveta, mradi wa unyunyuzaji maji wa Rombo, na mradi wa Nyumba za Bei Nafuu huko Loitoktok. Pia atakagua soko la kisasa la Kimana, mradi wa umeme wa Namanga-Isinya na hosteli za wanafunzi huko Kajiado.