Baraza la kitaifa la makanisa nchini NCCK linawaonya wanasiasa dhidi ya uchochezi wa kikabila na matamshi ya chuki kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao. Katibu Mkuu Chris Kinyanjui anasema uhuru wa kujieleza hauhusiani na matamshi yanayochochea hisia kali na yanaweza kusukuma Kenya kuelekea marudio ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007. Anasema wanasiasa hawapaswi kuogopa uchaguzi, bali wawaruhusu wapiga kura kuwawajibisha, iwe wanashinda au wanashindwa.
CHRIS KINYANJUI – INCITEMENT