Karibu mtoto mmoja kati ya watano wenye umri wa miaka 12 hadi 17 katika nchi 21 alipitia unyanyasaji au dhulma za kingono unaowezeshwa na teknolojia katika mwaka mmoja, kulingana na shirika la la UNICEF. Shirika hilo linakadiria kuwa takriban watoto milioni 20 waliathiriwa, wakiwemo zaidi ya milioni 15 walioathiriwa na maudhui ya ngono yasiyotakikana. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell anasema matokeo hayo yanaonyesha ukweli unaouma na yanatoa wito wa hatua kali zaidi za kuwalinda watoto mtandaoni.