Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua ametilia shaka uchunguzi wa polisi kuhusu kutekwa nyara kwa mhariri msaidizi wa Standard Group Alex Kiprotich. Gachagua anadai uchunguzi huo hautatoa matokeo kwa sababu polisi hawawezi kuwachunguza wenzao. Anadai utekaji nyara huo unahusishwa na taarifa ya uchunguzi aliyopanga kufanya Kiprotich kuhusu fidia ya waliofurushwa katika Msitu wa Mau. Gachagua amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kutoa matokeo ya uchunguzi wa awali kuhusu kesi zingine zinazodaiwa.