Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amehimiza vyombo vya habari kukuza ushiriki wa taarifa kwa uwajibikaji kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Ethekon anaonya dhidi ya taarifa potofu, zisizo na uhakik na mbaya, akisema ripoti za uchochezi zinaweza kuongeza hofu na shauku za umma na kutishia usalama wa taifa. Anasema vyombo vya habari lazima vitambue jukumu lake katika kuunda mazingira mazuri ya uchaguzi wa amani, unaoaminika, huru na wa haki, huku wadau wote wakizingatia utawala wa sheria.
ERASTUS ETHEKON - MEDIA